Home » » SITTA AWATAKA WAKINA WARIOBA WA WAACHIE WANANCHI KATIBA PENDEKEZWA WAAMUE WENYEWE

SITTA AWATAKA WAKINA WARIOBA WA WAACHIE WANANCHI KATIBA PENDEKEZWA WAAMUE WENYEWE


SITTA AWATAKA WAKINA WARIOBA WA WAACHIE WANANCHI KATIBA PENDEKEZWA WAAMUE WENYEWE
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba Mh.Jaji Joseph Warioba ni sahihi na kwamba kujitakia mwenyewe.
Akihojiwa na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa aliyofanyiwa Jaji Warioba ikidaiwa kuongozwa na Paul Makonda, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa hivyo hawako tayari kuona akina Warioba wanawapotosha.
Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea kufanya midahalo ya kupinga Katiba anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa pale Blue Pearl Hotel.
Pia amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.
Ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo na kukushughulikia. Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.
Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta alicheka na kusema hatajibu swali hilo.
Share this article :